Chelsea imemchukua mshambuliaji wa Brazil Alexandre
Pato kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 26 ambaye amekuwa
akichezea klabu ya Corinthians ya Ugiriki amechezea taifa lake mechi 27 na
kuwafungia mabao 10.
Alichezea Brazil katika Michezo ya Olimpiki mwaka
2008 na 2012.
Pato amesema anafurahi sana kujiunga Chelsea kwa
sababu ni timu aliyoitamani sana na anasubiri kuwafahamu wachezaji wenzake
wapya.
0 comments:
Post a Comment