Shirikisho la soka duniani FIFA limelegeza adhabu ya
vilabu vya Real Madrid na Atletico na sasa zipo huru kusajili hadi rufani zao
zitakapo sikilizwa na shirikisho hilo.
Klabu zote mbili ziliandika katika taarifa zao kuwa
FIFA wameziachia huru kuendelea na usajili wa wachezaji mara baada ya kufungia
kufanya hivyo kutokana na kufanya usajili wa watoto, kinyume na utaratibu.
Real Madrid na Atletico wote waliwasilisha rufani
zao kwa shirikisho hilo na sasa wataendelea kuwa huru hadi hapo FIFA
itakapopitia upya kesi yao na kufanya maamuzi.
Adhabu kama hiyo iliwakumba FC Barcelona mwaka 2014
na kufeli katika rufaa yao, kitu kilichopelekea
klabu hiyo isajili wachezaji Arda Turan na Alex Vidal ambao imeanza kuwatumia
mwezi huu wa January mara baada ya kumaliza kifungo.
0 comments:
Post a Comment