AZAM KUANZA KAZI LEO HUKO ZAMBIA


Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB, itaanza kuwania taji la mashindano maalum ya Zambia leo saa 10.00 jioni kwa saa za hapa kwa kucheza na Mabingwa wa Zambia na wenyeji wao, Zesco United mchezo utakaotanguliwa na ule wa ufunguzi utakaoanza saa 8.00 mchana baina ya Zanaco FC ya huko na mabingwa wa Zimbabwe Chicken Inn.

Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati watateremka tena dimbani saa 8.00 mchana Jumamosi ijayo kwa kukipiga na mabingwa wa Zimbabwe Chicken Inn, huku ukifuatiwa na ule baina ya wapinzani wa nchini humo Zesco na Zanaco utakaopigwa saa 10.00 jioni.

Azam FC itamalizia mechi yake ya mwisho Februari 3 mwaka huu kwa kukipiga na Zanaco, mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni, utakaotanguliwa na ule baina ya Zesco na Chicken Inn utakaoanza saa 8.00 mchana kabla ya siku inayofuata Februari 4 kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.

PICHA ZA AZAM IKIWA ZAMBIA


Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment