Mchezaji nambari moja duniani kwa upande wa wanawake
Serena Williams yuko mbioni kuandikisha rekodi ya kuwa mwanamke aliyewahi
kushinda michuano mingi zaidi duniani endapo atashinda fainali ya wanawake ya
mchuano wa Australian Grand Slam siku ya Jumamosi.
Mmarekani huyo alijiweka katika nafasi nzuri ya
kuweka historia baada ya kumbwaga Agnieszka Radwanska seti mbili kwa nunge za
alama 6-0, 6-4 katika hatua ya nusu fainali.
Mechi hiyo ya nusu fainali imechezwa mapema leo na
ilikuwa ni ya kupendeza.
Endapo Williams ataibuka mshindi dhidi ya mchezaji namba
ya 7 duniani Angelique Kerber, basi atakuwa ameshinda mashindano 22 makubwa ya
tenisi ya wazi na kufikia rekodi iliyowekwa na Steffi Graf aliposhinda mataji
22.
Vilevile atakuwa amempiku graf na kuwa mwanamke wa
pili baada ya Margaret Court aliyeandikisha rekodi ya kushinda mataji 24.
Williams anapigiwa upatu kundeleza msururu wa
matokeo mema hususan ikikumbukwa kuwa ameibuka kidedea katika mechi 6 za
fainali zilizoandaliwa katika ukumbi wa Melbourne Park nchini Australia.
Mpinzani wake Kerber alimuondoa muingereza Johanna
Konta katika hatua ya nusu fainali aliomlaza seti mbili kwa nunge za alama 7-5,
6-2 na kujikatia tikiti ya fainali yake ya kwanza ya Grand slam.
Kwa upande wake Kerber anatafuta ushindi wake wa
pili dhidi ya Williams tangu mwaka wa 2012.
0 comments:
Post a Comment