Serena Williams ametinga nusu fainali ya michuano ya
Australian Open kwa kumtwanga mpinzani wake mkubwa Maria Sharapova.
Mechi hiyo ilichezwa alfajiri ya leo huko nchini
Australia na kuhudhuriwa na mashabiki wengi.
Serena raia wa Marekani amemshinda kwa ulaini
Sharapova huku akimfunga kwa seti mbili mfululizo za pointi 6-4, 6-1 na
kumpeperusha nje ya michuano hiyo.
Ilionekana lilikuwa pambano rahisi kwake baada ya
kuibuka na ushindi huo ndani ya saa moja na dakika 32 tu.
Hata hivyo, Serena na Sharapova walilalamika hali ya
hewa kuwa ya joto kupindukia katika jiji la Melbourne.
0 comments:
Post a Comment