Kiungo wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Chelsea,
Ramires anakaribia kujiunga na timu ya Jiangsu Suning ya China.
Kiungo huyo mwenye miaka 28 alisajiliwa na Chelsea
toka Benfica, mwaka 2010 kwa dau la pauni milion 17 na inatarajiwa timu hiyo
inayocheza ligi kuu ya China iko tayari kutoa dau la pauni million 25 kumnasa
nyota huyo.
Ramires, alisaini mkataba mpya wa miaka minne mwezi
Octoba,mwaka jana, ila ameanza kikosi cha kwanza kwenye michezo saba tu msimu
huu wa ligi ya England.
Timu ya Jiangsu ilimaliza katika nafasi ya nane
kwenye msimu wa mwaka 2015, na kikosi hicho kinanolewa na nyota wa zamani wa
Chelsea Dan Petrescu.
Kiungo huyu wa kibrazil akiwa na The Blues, ametwaa
ubingwa wa ligi, kombe la FA, Kombe la Ligi, ubingwa wa klabu bingwa Ulaya na
ile michuano ya Europa Ligi.
0 comments:
Post a Comment