VIDIC SASA 'GARI LA MKAA'

Aliyekuwa beki wa klabu ya Manchester United ya England, Nemanja Vidic ametangaza kustaafu kutoka kandanda akiwa na umri wa miaka 34

Vidic alishinda mataji matano ya Premier League na Kombe la Mabingwa Ulaya mwaka wa 2007-2008 wakati wa miaka yake minane uwanjani Old Trafford, lakini akakumbwa na majeraha yaliyomlazimu kuamua kuzitundika njumu.

Mserbia huyo aliruhusiwa kuondoka klabu yake ya Inter Milan mapema mwezi huu baada ya kipindi cha miezi 18 nchini Italia iliyojaa majeraha. Vidic alijiunga na United akitokea Spartak Moscow mnamo Januari 2006 na akaweka ushirikiano imara katika safu ya ulinzi na Rio Ferdinand.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment