DERBY YAMNUSURU VAN GAAL KUTIMULIWA

Baada ya ushindi wa mabao 3-1 iliopata klabu ya Manchester United dhidi ya Derby County jana usiku kocha wa Man United Lois Van Gaal amesema timu yake imecheza vizuri kuliko walivyofanya mazoezi.

“Inawezekana tumecheza vizuri kuliko hata tulivyofanya mazoezi. Tulicheza vizuri kwa wakati muafaka dhidi ya Derby. Tuliruhusu goli lao lakini wakati wa mapumziko niliwaambia wachezaji walicheza kwa kiwango kizuri na waendelee kucheza kwa kiwango hicho tutashinda. Na tikawa hivyo”.

“Goli la Daley Blind lilikuwa goli zuri, unatakiwa kunusa ili kufunga goli la namna ile na yeye nadhani alinusa kujua kama kuna goli. Ligi kuu ni muhimu sana lakini kombe la FA ni kombe muhimu pia England lenye historia kubwa. Hatujashinda kombe hilo kwa muda mrefu kwa hiyo tunaliota. Baada ya ushindi wa mechi  mbili huwezi kusema utachukua kombe hilo”.

Magoli ya jana usiku kwa upande wa Manchester United yalifungwa na Wayne Rooney, Juan Mata na Daley Blind wakati goli la kufutia machozi kwa upande wa Derby lilifungwa na Thome.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment