YANGA NA AZAM FC 'MUZIKI MNENE' LEO

Timu za soka za Yanga na Azam FC usiku wa leo(Jumanne) zitashuka kwenye uwanja wa Amaan kumenyana katika mchezo wao wa pili wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Yanga inaikabili Azam huku ikiwa tayari ina pointi tatu na mabao matatu ya kufunga baada ya ushindi wa 3-0 iliyoupata juzi dhidi ya Mafunzo.

Azam FC itashuka dimbani huku ikiwa na pointi moja iliyopata juzi baada ya sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar.

Mechi hiyo huenda ikavuta hisia za wengi huko Zanzibar kufuatia timu hizo kubadilishana nafasi ya kwanza na ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu bara.

Mchezo huo ambao utaanza saa 2:15 usiku utatanguliwa na mchezo kati ya Mtibwa na Mafunzo ambao utaanza saa 10:15 jioni.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment