MCHEZAJI ALIYEMTONGOZA MWANAHABARI AADHIBIWA

Nahodha wa zamani wa timu ya kriketi ya West Indies, Chris Gayle amepigwa faini kwa kosa la kumtongoza mwanahabari wakati wa mahojiano ya moja kwa moja.

Gayle amepigwa faini ya dola 10,000 za Australia (sawa na $7,200; £4,900) na klabu yake ya Melbourne Renegades inayocheza ligi ya Big Bash.

Mchezaji huyo alimuuliza mwanahabari wa kipindi cha Ten Sport Bi Mel McLaughlin kama wangeweza kwenda faragha alipokuwa akihojiwa wakati wa mechi ya ligi dhidi ya Hobart Hurricanes Jumatatu.

"Kuyatazama macho yako mara ya kwanza kabisa ni jambo njema sana. Natumai tunaweza kuketi na kunywa kinywaji pamoja. Usione haya mtoto," alimwambia.

Baadaye, amejitetea na kusema alikuwa tu anafanya mzaha.

Chris Rogers, aliyekuwa nahodha wa Sydney Thunder wakati Gayle alikuwa mchezaji wa kawaida ameambia shirika la habari la ABC Grandstand kwamba hajashangazwa na kitendo hicho cha Gayle.

Gayle, 36, ni mzaliwa wa Jamaica lakini huchezea West Indies
Klabu ya Melbourne Renegades imesema matamshi hayo yalikuwa hayafai kabisa na yalikuwa ya “kuvunja heshima”.

Maafisa wa klabu hiyo wameomba radhi kwa McLaughlin na umma pia.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment