Timu za taifa za Mali na Congo DR kesho zitashuka
dimbani kucheza mchezo wa fainali wa michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani
CHAN.
Mali itamenyana na Kongo (DRC) katika kuanzia Saa
12:30 jioni kwenye Uwanja wa Amahoro,Rwanda, wakati Ivory Coast itamenyana na Guinea
kuwania nafasi ya tatu kwenye Uwanja huo huo kuanzia saa 9:00 Alasiri.
DRC ilitinga fainali baada ya kuifunga Guinea kwa
penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 kwenye uwanja wa Amahoro
pia.
Mali imefanikiwa kuingia Fainali ya Michuano ya
Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Ivory
Coast.
0 comments:
Post a Comment