SAMATTA ACHEZA LIGI ULAYA KWA MARA YA KWANZA

Mshambuliaji wa Kitanzania Mbwana Samatta usiku wa jana ameanza rasmi kazi huko Ulaya kwa kucheza mechi yake ya kwanza kabisa ya Ligi Kuu ya Ubelgiji wakati Genk ilipokwaana na Moeskroen.

Kwenye mechi hiyo Genk ilishinda bao 1-0.

Samatta ambaye ni mwanasoka bora Afrika ameichezea Genk kwa dakika 17.

Samatta aliingia katika dakika ya 73 katika mechi hiyo ya ugenini akichukua nafasi ya en Karelis.

Tayari wakati huo, Genk ilikuwa inaingoza kwa bao moja lililofungwa na Buffel katika dakika ya 62 na lilidumu hadi mwisho wa mchezo.

Kabla ya hapo, Samatta alipewa nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi cha akiba, kabla ya kupelekwa katika kikosi cha kwanza.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment