Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jana imejikatia tiketi ya kutinga hatua ya fainali ya michuano ya CHAN baada ya
kuilaza Guinea penati 5-4.
Mechi hiyo ya nusu fainali ilikuwa imekwisha kwa sare
ya bao 1-1 katika muda wa ziada baada ya Ibrahim Sankhon kuisawazishia Guinea
kunako dakika ya mwisho ya kipindi cha pili cha muda wa ziada.
Lakini dalili za kufuzu zilionekana mapema pale Ibrahim
Bangoura alipokosa penalti ya kwanza ya Guinea.
Katika penati Kimwaki, Mika, Jonathan Bolingi, Gikanji
na Mechak Elia waliifungia Leopards ya DRC huku Ibrahim Sankhon,Leo Camara,Kile
Bangoura na Daouda Camara waliifungia Guinea.
Hata hivyo Kipa nambari moja wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo Vumi Ley Matampi aliokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Youla na kuipa
DRC ushindi wa mabao 5-4.
0 comments:
Post a Comment