Tanzania imeendelea kupanda kidogo kidogo katika
viwango vya ubora wa soka duniani vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la
soka duniani FIFA baada ya kushika nafasi ya 125.
Kwa mujibu wa viwango vipya vilivyotolewa leo,
Tanzania imepanda kwa nafasi moja baada ya mwezi Disemba kushika nafasi ya 126.
Licha ya kupanda, Tanzania bado imeendelea kuburuzwa
na nchi za Afrika Mashariki.
Kenya ipo katika nafasi ya 99 baada ya kupanda kwa
nafasi mbili huku Uganda ikiwa inashika nafasi ya 70 baada ya kuporomoka kwa
nafasi nane.
Rwanda ipo nafasi ya 85 ikiwa safari hii imepanda kwa
nafasi sita wakati Burundi ikiwa kwenye nafasi ya 119 baada ya kupanda kwa
nafasi tisa.
Kwa ujumla nchi za Afrika Mashariki zinaburuzwa na
Uganda inayoshika nafasi ya 70.
FIFA imekuwa ikiangalia vitu vingi ikiwemo timu
kushinda ugenini ambapo pointi huongezeka zaidi ikilinganishwa na ushindi wa
nyumbani.
Kingine kinachoangaliwa na kuzingatiwa ni uwepo wa
mechi wanazozitambua iwe za kirafiki ama za mashindano ambapo kwa mwezi
uliopita Taifa Stars haikucheza mechi yoyote.
0 comments:
Post a Comment