MAN UNITED YALALA EUROPA LEAGUE

Manchester United walijikwaa katika juhudi zao za kufana Ulaya baada ya kushindwa ugenini na klabu ndogo kutoka Denmark katika Europa League.

United walichapwa mabao 2-1 na timu ndogo ya Midtjylland. Klabu hiyo ilianzishwa 1999.

Klabu hiyo ya Old Trafford pia ilipata pigo baada ya kipa wake namba moja David de Gea kuumia kufundo cha mguu wakati akipasha mwili moto na nafasi yake kuchukuliwa na Kipa wa Argentina Sergio Romero.

Man Utd walitangulia kufunga kupitia Memphis Depay lakini Midtylland wakasawazisha kupitia Pione Sisto.

Manchester United walishindwa na Sunderland 2-1 Jumamosi Ligi ya England na wamepungukiwa na alama sita kufikia nambari nne, nafasi ya kufuzu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Matokeo mengine ni:
Tottenham 1-1 Fiorentina
Valencia 6-0 Rapid Vienna.
Liverpool 0-0 Augsburg.
Anderlecht 1 –0 Olympiakos
Sevilla 3- 0 Molde
St Etienne 3-2 Basel
Villarreal 1- 0 Napoli
FC Sion 1-2 Sporting Braga
Galatasaray 1-1 Lazio
Marseille 0-1 Ath Bilbao
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment