YANGA 'WATIA KUFULI' MIDOMO YAO

Viongozi na wachezaji wa timu ya Yanga wiki hii wamekubaliana kutozungumza na vyombo vya habari hadi watakapocheza na Simba hapo kesho.

Huo ni utaratibu mpya ambao Yanga walianza nao tangu mechi yao iliyopita ya watani wa jadi ambayo Yanga ilishinda 2-0.

Yanga iliweka kambi kisiwani Pemba tangu Jumapili na hata walipotafutwa kuzungumzia maandalizi simu zao zilikuwa zikiita bila kupokelewa.

Habari za uhakika zinaeleza kwamba Yanga itarejea Dar es salaam leo ikitokea Pemba kwa ajili wa mechi ya kesho.

Kwa upande wao Simba, viongozi wao wamekuwa hawana tabu kuzungumzia maandalizi yao.

Timu hizo zitashuka kwenye uwanja wa taifa kesho Jumamosi.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment