MPINZANI WA CHEKA KUTUA LEO

Bondia Mserbia, Gerad Ajetovic anatarajiwa kutua Dar es Salaam leo Jumatano kwa ajili ya pambano la ngumi za kulipwa dhidi ya Mtanzania, Francis Cheka Februari 27, mwaka huu kuwania ubingwa wa Mabara wa WBF.

Meneja wa Cheka, Juma Ndambile amesema Rais wa WBF, Goldberg Haward na timu yake wasimamizi wa pambano hilo wanatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi.

Amesema Ajetovic atatua nchini majira ya saa nane mchana na kuwaomba Watanzania waende kumlaki kwa kumzomea ili kumchanganya.

Ndambile pia amesema Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni katika pambano hilo la raundi 12, uzito wa Super Middle litakalofanyika viwanja vya Leaders, Kinondoni mjini Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment