Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil na klabu
ya Barcelona, Neymar anatarajiwa kutoa ushahidi katika mahakama moja nchini
Hispania kuhusu madai ya ufisadi yanayozunguka uhamisho wake.
Aliyekuwa rais wa Barcelona Sandro Rossel na rais wa
sasa Josep Maria Bartomeu wamekana kufanya makosa yeyote katika uhamisho wa
nyota huyo jana.
Barcelona ilidai kulipa kiasi cha euro milioni 57
katika usajili wa Neymar mwaka 2013 huku wazazi wake nao wakipokea euro milioni
40 na klabu ya Santos aliyotokea wakichukua euro milioni 17.
Uchunguzi umebaini kuwa ada ya nyota huyo ilifikia
karibu euro milioni 83 na Barcelona wakituhumiwa kuficha kiasi kikubwa cha
mkataba huo.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na kampuni ya
uwekezaji ya DIS ambayo ilimiliki asilimia 40 ya haki za nyota huyo wakidai
kupunjwa haki yao kwa kuambulia euro milioni 6.8 kati ya euro milioni 17
walizopewa Santos.
0 comments:
Post a Comment