Gazeti la Daily Express limeripoti kuwa Chelsea
wapo kwenye mpango wa kumyakua kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini.
Pellegrini mwenye uraia wa Chile, ambaye anataraji
kufikisha miaka 63 baadaye mwaka huu, amesema kuwa ataondoka kunako klabu ya
City mwishoni mwa msimu, huku nafasi yake ikitarajiwa kujazwa na kocha wa
sasa wa Bayern Munich Pep Guardiola.
Kwa mujibu wa Pellegrini, bado yuko tayari
kusikiliza ofa kutoka sehemu mbalimbali kabla ya kuamua kustaafu rasmi
kufundisha soka, huku Chelsea wakionekana kama klabu namba moja kwenye mbio za
kumwania kocha huyo.
0 comments:
Post a Comment