Kocha Muhispania Pep Guardiola ametia saini mkataba
wa miaka mitatu kunako klabu ya Manchester City.
Guardiola, atachukua majukumu hayo kuanzia Julai,
klabu hiyo ya Ligi ya Uingereza imetangaza leo.
Manuel Pellegrini ataondoka klabuni hapo Juni 30
baada ya kumalizika kwa msimu wa sasa.
Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa kutokana na
heshima yao kwa Manuel Pellegrini na wachezaji, klabu ingependa kufanya wazi
uamuzi wake ili kuondoa nafasi ya uvumi.
Kumekuwa na uvumi kwa muda mrefu kwamba pengine
Guardiola angekwenda Manchester United ama Chelsea pindi msimu utakapomazilika.
0 comments:
Post a Comment