Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Lionel Messi
ameomba kukutana na mtoto Murtaza Ahmadi raia wa Afghanistan baada ya kuguswa
na picha aliyosambaza mitandaoni ikimuonesha akiwa amevaa mfuko wa plastiki
ulioandikwa jina lake.
Picha hiyo ilisambaa mnamo mwezi Januari ikionesha
ubunifu wa mtoto huyo ambaye alivaa mfuko wenye mistari ya bluu mpauko na
kuanika jila la Messi na namba tisa na kufanya ionekane kama jezi ya Argentina.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitano anatokea
Afghanistan vijijini.
Jumapili tovuti ya michezo ya Argentina TYC
ilithibisha kwamba Messi amezipata picha za Murtaza na amepanga kukutana na
kijana huyo.
Murtaza, ambaye anaishi Ghazni, Kusini mwa
Afghanistan ameshatafutwa kwa ajili ya kukutana na Messi.
Kwa sasa bado haijapangwa siku wala saa ambapo pande
mbili hizo zitakutana.
Afisa habari wa shirikisho la soka la Afghanistan,
Syed Ali Kazemi,
ametangaza kwamba: “Uongozi wa Afghan Football Federation
(AFF) umepokea email kutoka kwa Lionel Messi na Barcelona kuhusu Messi kukutana
na Murtaza”.
Xxxxx
0 comments:
Post a Comment