Klabu ya soka ya Simba imefuata nyayo za Azam FC kwa
kuzindua rasmi duka la kuuza bidhaa zake mbalimbali.
Duka hilo linamilikiwa na Insight Media ambao
watakuwa wanauza bidhaa za klabu za Simba.
Duka hilo liko Dar Free Market na litakuwa likiuza
vitu hivyo kwa bei nafuu na onyo limetolewa kwa wanaouza bidhaa feki.
Wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Rais wa Simba,
Evans Aveva aliwashauri Wanasimba wenye uwezo kujitokeza ili wapewe tenda ya
kusaidia kuuza vifaa vya michezo.
Mwezi Novemba mwaka jana klabu ya Azam FC ilizindua
duka la vifaa vya michezo maeneo ya Kariakoo jijini Dar es salaam kwa lengo la
kuondokana na bidhaa feki.
0 comments:
Post a Comment