TFF YAGUSWA NA KIFO CHA FRED MOSHA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa familia ya mwandishi wa habari za michezo Fred Mosha kilichotokea jana alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Katika salamu hizo, TFF imewapa pole familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki kufuatia kifo hicho, na kusema wapo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Fred Mosha mpaka umauti unamfika, alikuwa mkuu wa kitengo cha habari cha Tv/Redio Tumaini iliyopo jiini Dar es salaam na msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Mbagala Saku kwa Mkongo.

Mazishi yanatarajiwa kufayika kesho Jumatatu saa 9 mchana katika makaburi ya Kinondoni.

Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment