YANGA YATUA VISIWANI ZANZIBAR

Kikosi cha timu ya soka ya Yanga leo kimewasili visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba utakaochezwa Jumamosi ya Februari 20 mwaka huu.

Yanga ambayo jana ilikuwa Mauritius kucheza mchezo wa kwanza wa Klabu bingwa Afrika dhidi ya wenyeji Cercle de Joachim, imetua Zanzibar leo saa 4:40 asubuhi.

Jana Yanga iliifunga Cercle bao 1-0 na mchezo wa marudiano utachezwa wiki mbili zijazo jijini Dar es salaam.

Yanga imeonekana kuipenda kambi ya visiwani humo baada ya mwaka jana kuifunga Simba mabao 2-0 ikitokea huko.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment