![]() |
| Mashabiki wa Liverpool wakitoka uwanjani kabla ya mchezo kumalizika hapo jana |
Baadhi ya mashabiki wa Liverpool jana walimuacha
peke yake kocha wao Jurgen Klopp mara baada ya mlinzi wa Crystal Palace, Scot
Danny kufunga goli la ushindi katika dakika ya 82 ya mchezo na kufanya matokeo
kuwa 2-1.
Hicho ni kipigo cha kwanza kwa kocha Jurgen Klopp
tangu atue Liverpool hivi karibuni kuchukua mikoba ya Brendan Rogders
aliyetupiwa virago mwezi uliopita.
Akielezea tukio hilo mara baada ya mchezo, kocha
huyo raia wa Ujerumani alisema amesikitishwa sana na kitendo hicho cha
mashabiki kumkimbia na kumuacha peke yake wakati timu ikihangaika kurudisha
bao, hali anayoisema kuwa alijihisi mpweke zaidi na kusikitishwa sana na tukio
hilo.
Klopp amewataka mashabiki kuwa wavumilivu na kwamba
haipendezi kutoka uwanjani kabla ya dakika ya mwisho kwani kwenye mpira lolote
linaweza kutokea na kwamba ni vizuri kuisapoti timu hadi mwisho.
Aidha katika tukio jingine, Klopp alishuhudia kuumia
vibaya kwa mlinzi wake wa kati Mamadou Sakho ambaye leo atafanyiwa scan kuona
ni muda gani atakua nje ya uwanja.

0 comments:
Post a Comment