Messi |
Kocha mkuu wa klabu ya Barcelona
Louis Enrique ataamua saa moja kabla ya mchuano wa El Classico iwapo nyota wa
timu hiyo Lionel Messi atacheza dhidi ya Real Madrid au la baada ya kupona
jereha.
Real Madrid ambayo itaipiku Barcelona
katika kilele cha ligi hiyo iwapo itashinda ina kikosi kamili.
''Tunajua kwamba hatokuwa asilimia
100.Iwapo atacheza au la,habari njema ni kwamba amepona jeraha'',alisema
Enrique.Sijapanga lolote.Nitazungumza na leo siku ya Jumamosi .Saa moja kabla
ya mechi hiyo ya kukata na shoka tutaamua'
Mshambuliaji wa Real Madrid Karim
Benzema,ambaye anachunguzwa kwa kuhusishwa na usaliti wa kanda ya ngono na
ambaye anasema kuwa hakuhusika katika kashfa hiyo amekosa mechi sita kutokana
na jeraha.
''Benzema yupo katika
kikosi,alifanya mazoezi vizuri na ni miongoni mwa kikosi changu'',Meneja wa
Real Madrid Rafael Benitez alisema.''Bado tunajadiliana iwapo ataanzishwa au
la''.
Benzema |
0 comments:
Post a Comment