Mutasim |
Rais wa Chama cha Soka cha Sudan (SFA), Dk Jaffar
Mutasim, amechaguliwa kuwa rais mpya wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika
Mashariki na Kati (Cecafa), jana akichukua nafasi ya Leodegar Tenga wa
Tanzania.
Mutasim amechaguliwa kuchukua nafasi hiyo kutoka kwa
Tenga ambaye alikaa madarakani tangu mwaka 2007.
Tenga ameongoza Cecafa kwa vipindi viwili vya miaka
minne-minne.
Katika uchaguzi uliofanyika jana huko Ethiopia,
Mutasim alipata kura sita kati ya 10 zilizopigwa na kuwapiku wapinzani wake
Mganda, Lawrence Mulindwa aliyepata tatu na Mrwanda Vincent Nzamwita (1) na
Juneid Bashar Tilmo wa Ethiopia aliyejitoa.
0 comments:
Post a Comment