Ikiwa imepita miezi mitatu tangu aondoke Chelsea, daktari
wa wachezaji Eva Carneiro amefunga ndoa na mpenzi wake Jason De Carteret ambaye
ni mshauri na mtafiti wa mambo ya biashara.
Ndoa hiyo ambayo ilifungwa kwenye kanisa la St
Patrick mjini London, haikuhudhuriwa na
mchezaji, kocha wala kiongozi yoyote wa Chelsea.
Mchezaji aliyekuwepo kwenye harusi hiyo ni golikipa
wa zamani wa Chelsea Mark Schwarzer ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya
Leicester City.
Miezi michache iliyopita mrembo huyo alikwaruzana na
kocha Jose Mourinho na kutimuliwa katika klabu hiyo.
Mourinho alikorofishana na Eva kwa madai kwamba
alipoteza muda wakati anamtibu Eden Hazard huku Chelsea ikiwa tayari imefungwa.
Eva akikwaruzana na bosi wake Mourinho wakati alipokuwa Chelsea |
0 comments:
Post a Comment