KATIKA michezo, mpira unapoingia golini watu wote
hushangilia kwa sauti kubwa,
“Goooooooooo!”
Neno hilo limetokana na kifaa kinachowekwa katika
pande mbili za uwanja, ambazo ndizo tendo la ufungaji linatendeka.Kifaa hicho
kina utofauti wake kulingana na mchezo husika ambapo mchezo wa soka huwa
kunakuwa na milingoti mitatu iliyoungana inayosimikwa katika pande mbili za
uwanja.
Milingoti ya namna hiyo unaweza pia kuiona kwenye uwanja
wa mchezo wa mpira wa mikono, mpira wa magongo nk.Kadhalika katika mchezo wa
mpira wa kikapu, kifaa hicho huwa tofauti kidogo ambapo huwa na muonekano wa duara.
Kifaa hicho pia lazima ukikute katika mchezo wa
mpira wa pete ambapo pia huwa na umbo la duara.
ASILI
YA NENO ‘GOAL’
Bila kujali kinatumika kwenye mchezo gani, kifaa
hiki Waingereza walikipa jina la ‘Goal’ ambalo tafsiri yake ya kawaida ni
malengo yanayotimizwa kutokana na juhudi fulani.
Hivyo neno hilo likapelekwa kwenye michezo kwa maana
ya kwamba timu inapokuwa uwanjani lazima ifikie malengo kutokana na juhudi
inazoonyesha ndani ya uwanja.Hapo ndipo walipotafuta kifaa maalumu na kukipa
jina la goal kwa maana kwamba timu lazima ipitishe mpira katika sehemu husika
ili kupata suluhu ya juhudi zake.
Vinginevyo timu zote tunazoziona hivi sasa zingekuwa
zinapambana tu bila kupata mshindi na mwishowe hata mechi zingekuwa hazina
maana yoyote ile.
NENO
LIMETOHOLEWA
Mataifa mengi duniani yametohoa neno hili la
kiingereza kwenda katika lugha zao ili kupata urahisi wa kulitamka pindi mpira
unapoingia langoni.
Lakini licha ya kutohoa na kupata maneno
yanayoandikwa kwa lugha tofauti tofauti, matokeo ya mwisho ya utamkaji wake
huishia kufanana.
Mataifa yanayozungumza lugha ya kiingereza yakiwemo
ya Bara la Afrika, neno ‘goal’hulitamka “Gooooooooo!”. Ndivyo ambavyo pia
utasikia nchi kama Hispania, Denmark, Ujerumani pamoja na nchi zingine za Bara
la Amerika zikiwa zinatamka hivyo hivyo.
Nchi za Afrika Mashariki ambazo watu wake
wanazungumza lugha ya Kiswahili kama Tanzania, nayo imetohoa neno hilo na
kuliita ‘goli’.Mashabiki wanaposhangilia kufungwa kwa goli nao hutamka matamshi
yanayofanana na mataifa mengine, “Gooooooo!”
Kadhalika nchi kama Kenya na Uganda ambazo baadhi ya
watu wake wanazungumza lugha ya Kiswahili, nao linapofungwa goli hushangilia
kwa matamshi hayohayo.
GOLAZO
Golazo ni neno ambalo limejizolea umaarufu sana kwa
hivi sasa hasa katika nchi za Hispania, Brazil na Colombia.
Kwa mfano goli linapofungwa katika mechi ya mpira wa
miguu utasikia mtangazaji akitamka “Gooolaaazoooooooo!”
Lakini neno Golazo mara zote hutamkwa kifupi, yaani
“Goooooooooo” badala ya kumalizia ‘Golazooo’.
HELUWA
Neno hili linatumika sana katika nchi za kiarabu
hasa baada ya goli kufungwa ambapo watangazaji na mashabiki husikika wakisema
“Heluwaaaaaaaaa!”
Heluwa kwa kiarabu ni kitu kizuri sana, hivyo
inapotokea goli zuri limefungwa basi hutumia neno hilo.
Licha ya kutumia ‘Heluwa’, kuna wakati wanalazimika
kutamka neno “Goooooooooo!”.Mara nyingi haya maneno hutumika kwa pamoja hasa
goli linapofungwa katika mchezo wa soka.
Kwa ujumla ushangiliaji wa goli uwanjani
huwaunganisha watu pamoja na kuwa kitu kimoja kwa sababu wanatamka kitu
kinachofanana.Kwa muda huo hata ubaguzi huwekwa pembeni bila kujali kwamba neno
hilo huandikwaje.
Makala haya yameandaliwa na Arone Mpanduka kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vya mtandao wa Intaneti.
0 comments:
Post a Comment