Blatter(kushoto) na Platini(kulia) |
Rufaa iliyokatwa na Rais wa Shirikisho la soka
duniani FIFA Sepp Blatter na Michel Platini ya kupinga kifungo cha soka cha
siku 90 imekataliwa.
Adhabu hiyo ilitolewa mwezi Oktoba mwaka huu na kamati
ya maadili ya shirikisho hilo.
Blatter,Valcke na rais wa UEFA Platini walisimamishwa
na kamati hiyo ili kupisha uchunguzi kuhusu madai ya ufisadi.
Watatu hao wamepigwa marufuku kushiriki katika
michezo yoyote ya kandanda kwa muda huo.
Blatter anatuhumiwa kwa kutia saini kandarasi
isiyokuwa na umuhimu wowote kwa FIFA mbali na kutoa malipo kwa rais wa
shirikisho la UEFA Michel Platini kinyume na matakwa ya shirikisho hilo.
Kamati ya maadili pia ilianzisha uchunguzi dhidi ya
Platini kuhusu malipo hayo ya Yuro milioni 2 ambayo yalifanywa miaka minane
baada ya Platini kumfanyia kazi Blatter.
0 comments:
Post a Comment