Hali ya usalama kuelekea mchezo wa Jumamosi wa Clasico kati
ya Real Madrid na Barcelona umepangwa kuimarishwa maradufu kufuatia tukio la
mashabulio ya kigaidi lililotokea wiki iliyopita jijini Paris.
Mchezo huo wa La Liga utaangukia ikiwa imepita wiki
moja baada ya magaidi kushambulia maeneo kadhaa katika mji mkuu huo wa Ufaransa
na kuuwa watu zaidi ya 129 na kuacha wengine mamia majeruhi.
Mchezo huo wa Classico utakaochezwa katika Uwanja wa
Santiago Bernabeu hauko katika mashaka ya kutochezwa lakini polisi jijini
Madrid wataongezwa ili kuhakikisha usalama zaidi katika mchezo huo
utakaozikutanisha klabu kubwa duniani.
Polisi wamedai kuwa mpaka vyakula vitakaguliwa
wakati wa kuingia uwanjani hivyo kuwataka mashabiki kutoa ushirikiano katika
mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment