Pape N'daw |
Klabu ya soka ya Simba imeamua kuachana na wachezaji
Pape N’daw raia wa Senegal na Simon Sserunkuma kufuatia kuwa na mwenendo mbovu.
Akizungumzia kuachwa kwa wachezaji hao, Mkuu wa
Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu ya Simba Hajji Manara alisema
uongozi umeridhia na kuamua kuachana na wachezaji hao baada ya kupokea ripoti
ya kocha mkuu Muingereza Dylan Kerr.
Alisema pamoja na kuachana na wachezaji hao, klabu
yao ina mipango ya kuwaongeza wachezaji wengine akiwemo Paul Kiongera.
“Pape N’daw na mwenzake si kwamba ni wabaya, wazuri
lakini kuna wakati mchezaji anakuwa haendani na programu za kocha na huenda
hilo ndilo lililotokea kwao.Tunawashukuru sana wachezaji hawa kwa mchango wao,”alisema
Manara.
“Simon amekwishaondoka lakini N’daw bado yupo na
tunategemea siku hivi mbili tatu naye atarejea Senegal na jana tu alifanya
mazoezi ili kuuweka fiti mwili wake”
MATUKIO YA KUKUMBUKWA YA MSENEGALI PAPE N'DAW KWA NJIA YA PICHA
0 comments:
Post a Comment