Klabu ya Arsenal inajiandaa kumpa mkataba mpya wa
miaka mitano mchezaji wake Alexis Sanchez pamoja na Mjerumani Mesut Ozil ambao
wote wamebakiza misimu miwili na nusu kila mmoja huku klabu ikihofia kufanya
nao mazungumzo katika miaka miwili ya mwisho.
Alexis Sanchez ambaye analipwa pauni 130,000 kwa
wiki hivi sasa anatarajiwa kuongezewa hadi kufikia mshahara wa pauni 155,000
kwa wiki kama atasaini mkataba huo mpya wa miaka mitano.
Tayari mazungumzo baina ya maafisa wa klabu na
wawakilishi wa Sanchez yanaendelea na taarifa zinasema yanaendelea vizuri na
kwamba ni taarifa nzuri kwa kocha Arsene Wenger ambaye amekua akimtegemea zaidi
mchezaji huyo tangu atue Arsenal akitokea Barcelona.
Wakati huo huo Arsenal pia inajiweka sawa kumfunga
pia mjerumani Mesut Ozil ambaye naye amebakiza msimu miwili na nusu katika
mkataba wake wa sasa ambao ndio anaongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa wa pauni
140,000.
0 comments:
Post a Comment