Mkwasa(katikati)akizungumza na waandishi wa habari mapema leo.Picha kwa hisani ya TFF |
Na Nicolaus Kilowoko
Siku moja baada ya kikosi cha timu
ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kutolewa katika hatua ya kusaka tiketi ya
kushiriki fainali za kombe la dunia nchini Urusi, kocha mkuu wa timu hiyo
Charles Boniface Mkwasa amefunguka kuhusiana na kilichopelekea kupoteza mchezo
wao dhidi ya wapinzani wao Algeria.
Akizungumzia sababu za kutolewa
katika hatua hiyo Mkwasa alisema pamoja na kupoteza mchezo huo lakini
anawashukuru watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono katika kipindi
chote cha mashindano.
Lakini
amekiri kuwepo kwa mapungufu katika kikosi chake katika mchezo huo huku
akielezea ni kwa jinsi gani wapinzani wao walivyoungwa mkono na Serikali yao
kwa kipindi chote cha mchakato huo wa kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki kombe dunia .
Mkwasa alisema wenyeji wao
waliwatengenezea mizengwe kwa kipindi chote walichokuwa nchini Algeria huku
akidai kwamba matokeo waliyopata Algeria ya mabao 7-0 yalitokana na fitina
zilizofanyika kuanzia nje ya uwanja.
Alisema walifanyiwa vitendo ambavyo
vilisababisha kuwatoa mchezoni wachezaji wake na kupelekea kushindwa kufanya
vizuri katika mchezo huo.
“Pamoja na yote, ninawashukuru
Watanzania kwa sapoti kubwa walioionyesha kwetu tangu tulipokuwa kwenye
maandalizi hadi siku ya mchezo,”alisema Mkwasa.
Naye nahodha msaidizi wa Taifa Stars, John Bocco
ameishukuru TFF kwa kuwapatia huduma bora za maandalizi na wakati wa michezo
yao yote, amewashukru watanzania na vyombo vya habari kwa kuwapa sapoti na
kuwaomba kuendelea kuwaunga mkono pindi wanapokua na majukumu ya kuiwakilisha
nchi katika michuano mbalimbali.
“Matokeo ya juzi (dhidi ya Algeria) sisi wachezaji
yametusikitisha, tulikua na malengo na mtazamo tofauti wa kupata ushindi,
lakini katika mpira kuna matokeo matatu, tumepoteza mchezo huo kikubwa ni
kujipanga kwa ajili ya michezo ijayo na watanzania muendelea kutusapoti timu ya
Taifa kama ambavyo mmekua mkifanya kwa sasa” alisema Bocco.
Stars imerejea leo alfajiri ikitokea nchini Algeria
ilipokua na mchezo wa marudiano dhidi ya Algeria, Jumanne katika uwanja wa
Mustapher Tchaker mjin Bilda ambapo ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 7
-0.
0 comments:
Post a Comment