Mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale yu
katika hatihati ya kuipa kisogo Real Madrid kufuatia kichapo cha mabao 4-0
ilichopata timu yake kutoka kwa Barcelona.Inaelezwa kuwa Manchester United
inajiandaa kutenga dau kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji huyo.(The Sun)
Inaelezwa kuwa mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano
Ronaldo, 30, amekasirishwa na kichapo cha Jumamosi cha mabao 4-0 hivyo anataka
kocha wake Rafael Benitez aondolewe na nafasi yake ichukuliwe na mtu mwingine
(Daily Telegraph limeandika)
Bosi wa Liverpool Jurgen Klopp anataka kumsajili
kiungo wa Lazio Lucas Biglia mwenye umri wa miaka 29 lakini atakumbana na
ushindani kutoka Manchester United. (Fichajes - Hispania)
Klabu ya Southampton inataka kumshikilia
mshambuliaji wake Sadio Mane mwenye umri wa miaka 23 ili asiondoke na inataka
kumuongezea mkataba mpya ili kuzima mbio za Manchester United na Chelsea juu ya
mchezaji huyo. (Daily Express)
Klabu za Manchester United na Arsenal zinamuwania
beki wa Juventus Danile Rugani mwenye umri wa miaka 21.
0 comments:
Post a Comment