Ramos(kushoto) na Marcelo (kulia) |
Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos na mlinzi
mwenza, Marcelo wamewaomba mashabiki wa klabu yao ya Madrid kuwasamehe kutokana
na kipigo cha magoli 4-0 walichokipokea toka kwa mahasimu wao FC Barcelona
katika uwanja wa Santiago Bernabeu, mjini Madrid mwishoni mwa juma hili.
Ramos amesema, kama wachezaji, wanaomba radhi sana
kwa mashabiki wao kwa kilichotokea.
Amesema wanajua vitendo vina nguvu kuliko Maneno, hivyo
wanahitaji kuonesha uwanjani na kuwafariji mashabiki.
Aidha mlinzi wa kushoto wa klabu hiyo Mbrazil
Marcelo amesema hawakupoteza mchezo kwa sababu ya mashabiki huku wakisisitiza
kuwa morali iko juu na kwamba wanamuamini kocha wao Rafael Benitez ambaye hiyo
ilikua ni El Classico yake ya kwanza.
Akiunga mkono kauli hiyo ya Marcelo, kiungo Luka
Modric amesisitiza imani waliyonayo wachezaji kwa mwalimu wao Rafael Benitez,
huku akikazia kuwa hali yao kama wachezaji iko vizuri.
0 comments:
Post a Comment