Kuna tetesi kwamba klabu ya soka ya Azam FC inataka
kumsajili kipa Ivo Mapunda ambaye kwa sasa hana timu tangu alipotemwa na Simba
SC.Kwa muda mrefu Ivo amekuwa akifanya mazoezi na wachezaji wa Azam FC ili
kujiweka fiti.
Kuna tetesi kwamba klabu ya Simba inasikilizia
kumalizika kwa michuano ya Chalenji ili iweze kufanya mazungumzo ya kina na
mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya Paul Kiongera.
Pia klabu hiyo ina mpango wa kusajili wachezaji
wengine wawili zaidi ili kuimarisha kikosi chake.
Tetesi zingine zinadai kwamba Klabu za Toto
Africans, Stand United na Mbeya City zinamfukuzia mshambuliaji wa Yanga Simon
Matheo.
0 comments:
Post a Comment