Timu ya soka ya taifa ya Zanzibar maarufu kama Zanzibar
Heroes mchana wa leo(Novemba 24,2015) imepoteza tena mchezo wake wa pili wa
michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup baada ya kupokea kichapo kizito cha
mabao 4-0 kutoka kwa Uganda.
Katika mhezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la
Awassa huko nchini Ethiopia, Zanzibar Heroes imeshuhudia wachezaji wake wawili
wakilimwa kadi nyekundu.
Wachezaji hao ni golikipa Mwadini Ali(kadi dakika ya
14) na Mudathir Yahya(kadi dakika ya 75).
Mabao ya Uganda katika mchezo huo yamefungwa na
Farouk Miya aliyefunga mabao mawili ya mwanzo katika dakika za 10 na 14 huku
bao la tatu likifungwa na Erisa Ssekisambu(dakika ya 48) na la nne limefungwa
na Denis Okoth (dakika ya 78)
Kupoteza mchezo hii leo kwa Zanzibar kumeiweka
katika hali mbaya zaidi ya kufungasha virago kufuatia kushika mkia baada ya
kupoteza pia mchezo wake wa awali dhidi ya Burundi kwa kufungwa 1-0.
0 comments:
Post a Comment