Kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars Abdallah Kibadeni |
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars
jioni ya leo(Novemba 24,2015) imefanikiwa kuinyuka Rwanda Amavubi mabao 2-1
katika mchezo wa pili wa kundi A la michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup
inayoendelea nchini Ethiopia.
Katika mchezo huo ambao ulipigwa mjini Awassa, Kili
Stars ilitangulia kupata mabao mawili yaliyofungwa na Said Ndemla katika dakika
ya 22 ya mchezo pamoja na Simon Msuva aliyefunga katika dakika ya 78.
Bao la kufutia machozi la Amavubi lilifungwa na
Jaques Tuyisenge katika dakika ya 89.
Ushindi huo umefuta uteja kwa Rwanda ambayo mara kadhaa imekuwa kikwazo kikubwa cha Kilimanjaro Stars katika michuano hiyo.
Kufuatia ushindi wa leo,Kili Stars ambayo inanolewa
na babu Abdallah King Kibadeni Mputa, ipo kileleni mwa msimamo wa kundi A ikiwa
na jumla ya pointi 6 na mabao 6 ya kufunga na hivyo imefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
0 comments:
Post a Comment