Kavumbagu |
Kikosi cha Zanzibar Heroes leo kimeanza vibaya
mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup baada ya kuchapwa bao 1-0 na Burundi
kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la Addis Ababa nchini Ethiopia.
Bao hilo pekee limefungwa na mshambuliaji hatari wa
Burundi ambaye pia anakipiga katika klabu ya Azam FC Didier Kavumbagu.
Bao hilo ambalo lilipatikana katika kipindi cha
kwanza mnamo dakika ya 39 limeifanya Burundi kuanza vema ikiwa na pointi tatu kwenye kundi B.
Kesho Tanzania Bara itakipiga dhidi ya Somalia
majira ya saa 8 mchana.
0 comments:
Post a Comment