Ligi kuu soka nchini Uingereza itaendelea tena usiku
wa leo kwa mchezo mmoja mkali kati ya Leicester City dhidi ya Manchester City.
Mtanange huo utapigwa nyumbani kwa Leicester kunako
dimba la King Power huku wenyeji hao wakiwa wanashika nafasi ya pili kwa kuwa
na pointi 38 wakati Man City wakiwa nafasi ya nne na pointi zao 35.
YUPI
ANACHEZA NA YUPI HACHEZI?
Wapachika mabao wawili wa Leicester
Jamie Vardy naRiyad Mahrez ambao Jumamosi walifanyiwa mabadiliko kwenye dimba
la Anfield, usiku wa leo watakuwa tayari kushuka dimbani.
Naye Danny Drinkwater atakuwa tayari
kurejea dimbani.
Nahodha wa Manchester City Vincent
Kompany huenda asicheze leo baada ya kupatwa na jeraha la shingo kwenye mchezo
dhidi ya Sunderland.
Mshambuliaji Sergio Aguero leo
atarejea dimbani lakini Pablo Zabaleta na Fernando huenda wasicheze.
MAKOCHA
WANASEMAJE?
Kocha mkuu wa Manchester City, Manuel Pellegrini anasema
ni lazima waichukulie Leicester kama timu yenye uwezo wa kupigania taji la
ubingwa hadi mwisho wa msimu.
Amesema walikuwa kileleni mwa ligi na wanastahili kuwepo
mahali hapo.
Naye kocha mkuu wa Leicester, Claudio Ranieri
amesema kitendo cha kukumbana na Man City ni mtihani mwingine mkubwa lakini
lengo lake ni kushinda taji.
Mechi itapigwa saa 4;45 usiku kwa saa za Afrika
Mashariki.
0 comments:
Post a Comment