Denis Cheryshev |
Rufaa ya klabu ya Real Madrid ya kupinga kuenguliwa
katika michuano ya Kombe la Mfalme kwa kuchezesha mchezaji asiyeruhusiwa
imegonga mwamba.
Mabingwa hao mara 19 wa michuano hiyo walienguliwa
kwa kumchezesha winga Denis Cheryshev katika mchezo dhidi ya Cadiz uliochezwa
Desemba 2 mwaka huu.
Cheryshev alipaswa kutumikia adhabu yake kutocheza
mechi moja ambayo aliipata wakati akicheza kwa mkopo Villarreal msimu uliopita.
Mahakama ya Michezo ya Hispania ilitupilia rufani ya Madrid baada ya kusikiliza
maelezo ya pande zote kuhusiana na sakata hilo.
Madrid kwasasa wanashikilia nafasi ya tatu katika
msimamo wa La Liga nyuma ya mahasimu wao Barcelona na Atletico Madrid.
0 comments:
Post a Comment