DONALD NGOMA AING'ARISHA YANGA MAPINDUZI CUP

Yanga leo imeanza vema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuikung'uta Mafunzo ya Zanzibar mabao 3-0 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa kwenye dimba la Amaan visiwani humo.

Yanga ilipata mabao mawili kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Donald Ngoma katika dakika ya 31 na 34 huku mchezaji mpya aliyesajiliwa kutoka Mbeya City Paul Nonga akifunga la tatu katika dakika ya 89.

Kwa matokeo hayo Yanga inaongoza kundi ikiwa na pointi tatu na mabao matatu ya kufunga.

Mchezo mwingine utafuatia usiku huu kuanzia majira ya saa 2:15 kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment