FRANCIS CHEKA APEWA KIBARUA KINGINE

Bondia Francis Cheka, amepewa mtihani mwingine ambapo anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na bingwa wa Bara la Ulaya, Geard  Ajetovic raia wa Uingereza katika pambano la kugombania  mkanda wa ubingwa wa WBF  Intercontinental linalorajiwa kufanyika Februari 27, mwaka huu kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar.

Cheka ambaye hivi karibuni alipoteza dhidi ya Thomas Mashali katika pambano lisilokuwa la ubingwa lililofanyika mkoani Morogoro, atacheza pambano hilo huku akiwa na kumbukumbu ya kuwahi kuchapwa na bondia huyo mwenye asili ya Serbia katika pambano lililofanyika nchini Uingerezea miaka kadhaa iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Saalam, promota wa pambano hilo, Jay Msangi alisema kuwa pambano hilo la kugombania ubingwa ambalo ni maalum kwa ajili ya Cheka ili aweze kulipiza kisasi cha kupigwa na Muingereza huyo wa Ulaya, litasimamiwa na Shirikisho la Ngumi za Dunia WBF.

Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment