HAYA NDIYO MATOKEO YA AZAM NA MTIBWA USIKU HUU

Timu za Mtibwa Sugar na Azam FC usiku huu zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa pili wa michuano ya Mapinduzi.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Amaan, Mtibwa walianza kupata bao dakika ya 60 kupitia kwa Hussein Javu lakini mnamo dakika ya 74, John Bocco akaisawazishia Azam na kufanya 1-1.

Hata hivyo katika mchezo huo mashabiki waliofika uwanjani hapo walionekana kutofurahishwa na maamuzi wakidai kwamba muda mwingi alikuwa akiipendelea Azam FC.

Michuano hiyo itaendelea kesho(Jumatatu ya Jan 4)
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment