Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi
leo ameomba radhi kufuatia kitendo cha kuvuruga ratiba ya Ligi Kuu kwa kuiruhusu
timu ya Azam FC kwenda nchini Zambia.
Siku chache zilizopita TFF iliiruhusu Azam kwenda
nchini humo kushiriki mashindano maalum jambo ambalo litailazimu timu hiyo
ipangiwe mechi zake pekee za kiporo pindi itakaporejea nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo,
Malinzi amesema hana sababu ya kumlaumu mtu mwingine zaidi ya yeye mwenyewe kuwajibika
kufuatia nafasi yake kubeba jina la TFF.
Malinzi amekiri kwamba kitendo cha kuiruhusu Azam
iondoke wakati Ligi ikiwa inaendelea moja kwa moja kinaathiri ratiba.
“Hakuna haja ya kumsaka mchawi.Kosa ni la TFF na
muungwana akivuliwwa nguo huchutama.Mimi nakiri nimekosea na ninaomba radhi kwa
wadau wa soka,”alisema.
Malinzi amesema kufuatia hali hiyo, Azam itakaporejea
italazimika kucheza mechi mbili kila wiki ili kufidia mechi zake za viporo na pia
kwenda sambamba na timu zingine.
Amesema hiyo ndiyo itakuwa adhabu yao na wanaamini kwa
kuwafanyia hivyo hawawezi kulalamika.
“Wakati tulipopanga ratiba ya timu kucheza mechi moja
kila wiki, makocha wengi walitupongeza kwa kitendo hicho lakini kwa sasa Azam itakaporejea
hatutakuwa na huruma nayo,itacheza mechi mbili kila wiki wakati wenzao wakiwa
wanacheza moja kila wiki”
0 comments:
Post a Comment