Yanga SC leo hii imefunga safari kwenda jijini Tanga
kucheza mechi ya Ligi kuu Bara dhidi ya wenyeji Coastal Union itakayopigwa
Jumamosi wiki hii.
Yanga imefuta mpango wa kwenda nchini Afrika Kusini
kuweka kambi ya muda mfupi baada ya Azam kupewa ruhusa ya kwenda Zambia kucheza
mechi za mashindano maalum.
Yanga imefuta safari hiyo ya bondeni baada ya
Shirikisho la soka nchini TFF kuwanyima ruhusa ya kufanya hivyo.
“TFF imetunyima ruhusa kwa hiyo tunaenda Tanga,hivyo
kama Azam inataka kutumia mechi za viporo ili kupata ubingwa basi sisi
tutapambana nao kwa matokeo ya uwanjani,”alisema Jerry Muro ambaye ni Mkuu wa Kitengo
cha Habari na Mawasiliano cha Yanga.
Tayari Simba SC ilitangaza jana kwamba nayo haitoiga
safari ya Azam na badala yake itabaki nchini kucheza mechi za Ligi kuu.
Azam ambayo ipo Zambia jana ilitoka sare ya bao 1-1
na wenyeji Zesco United katika mchezo wake wa kwanza wa mashindano hayo maalum
na kesho itashuka tena dimbani.
0 comments:
Post a Comment