VAN GAAL YUPO YUPO SANA MAN U

Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal anataka kuendelea kubakia kuwa meneja wa Manchester United hadi mkataba wake utakapoisha kiangazi cha mwaka 2017 na hana mpango wa kujiuzulu hata kidogo.

Pamoja na presha kuwa kubwa zaidi kwa kocha kuyo kutokana na matokeo hasi ya timu yake tangu kuanza kwa msimu huu, lakini kocha huyo mwenye jeuri amesisitiza kuwa hakuwahi kufikiria kujiuzulu kibarua chake na kwamba siku zote amekua ni mpiganaji ili afaulu mitihani yake.

Kocha huyo amesema anashukuru sapoti kubwa anayoipata kutoka kwa makamu mwenyekiti wa timu hiyo Ed Woodward pamoja na wamiliki wa timu hiyo familia ya Glazer ambao anasema wanamfanya aongeze juhudi za kuirudisha timu katika mstari.

Kauli hizo za Louis Van Gaal ni za kuwakata maini wale wote waliopenda kocha Jose Mourinho ama Pep Guadiola watue Old Trafford kuchukua mikoba ya mholanzi huyo lakini sasa haijulikani ni lini ataondoka na kwamba anaweza kumaliza miaka yake yote mitatu.

Manchester United wanatarajia kuwafuata klabu ya ligi daraja la kwanza nchini England klabu ya Derby usiku wa leo katika mchezo wa chama cha soka nchini England, FA huku wakiwa na majeruhi 8 mara baada ya Matteo Darmian naye kuumia katika mchezo ulipita dhidi ya Southampton.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment