SIMBA, YANGA 'ZAIGA' SAFARI YA AZAM



Siku moja baada ya Azam kusafiri kwenda nchini Zambia kucheza mashindano maalum ya mualiko, hatimaye Simba na Yanga nazo zimeamua kufanya ziara zake za mazoezi.

Ligi kuu Tanzania Bara imepumzika kwa muda baada ya mechi za duru la kwanza kumalizika wiki iliyopita huku la pili likitarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii.

Wakati Ligi hiyo ikiwa kwenye mapumziko mafupi, michuano ya kombe la FA imekuwa ikiendelea kuchezwa.

Lakini Yanga imeibuka na kudai kwamba ipo mbioni kusafiri kwenda nchini Afrika Kusini kucheza mechi kadhaa za kirafiki ili kujiweka fiti zaidi.

Mkuu wa Kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amesikika akisema kwamba wataondoka nchini Ijumaa kwa ajili ya kambi hiyo.

Kambi ya Yanga inatarajia kuwa katika mji wa Johannesburg ambako itaweka kambi inayotarajiwa kuwa ya zaidi ya siku tano.

Kama hiyo haitoshi, kutoka kwa Simba SC kuna taarifa za uhakika zinaeleza kwamba nao wako mbioni kusafiri juma hili kwenda Kenya kwa ajili ya kushiriki mashindano maalum.

Simba itakwenda kushiriki mashindano ambayo yatajumuisha jumla ya timu nane.

IFUATAYO NI RATIBA YA LIGI KUU BARA AMBAYO HUENDA IKAATHIRIWA NA KUONDOKA KWA AZAM, YANGA NA SIMBA

VPL FIXTURES JAN 30,2016
Coastal Union    vs      Young Africans           16:00

Simba SC vs      African Sports    16:00

JKT Ruvu vs      Majimaji    16:00

Tanzania Prisons         vs      Azam FC 16:00

Mtibwa Sugar     vs      Stand United      16:00

Mwadui FC        vs      Toto Africans     16:00

Kagera Sugar      vs      Mbeya City         16:00
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment