Na Arone Mpanduka
Kocha mkuu wa Azam FC Stewart John Hall amesema katika mechi ya leo atatumia asilimia kubwa ya wachezaji chipukizi.
Usiku wa leo(Jumapili) Azam itashuka kwenye uwanja wa Amaan kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Akizungumza na MPANDUKA BLOG, Muingereza huyo alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwapumzisha nyota wake ambao wanakabiliwa na mashindano makubwa.
"Hutomuona Wawa, Bocco, Manula, Aggrey, Tchetche na wengineo.Wote nitawapumzisha na kuwatumia vijana"
"Tuna mashindano muhimu sana huko mbele kama vile Ligi ya Vodacom, Kombe la Shirikisho, Kombe la Kagame na Kombe la FA, kwa hiyo sitaki kuwachosha wachezaji wangu mapema,"alisema.
"Nini Mapinduzi Cup bwana, mashindano haya ni kama mazoezi tu, huwezi kufananisha na haya niliyokutajia"
Alisema atahakikisha wanacheza kwa tahadhari kubwa katika mashindano hayo.
Moja kati ya angalizo zilizotolewa na waratibu wa michuano hiyo ni timu kuhakikisha inatumia wachezaji wa kikosi cha kwanza ili kuongeza ladha ya mashindano.

0 comments:
Post a Comment